MATUMIZI YA LUGHA YA TAMATHALI ZA SEMI KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI: MIFANO KUTOKA DIWANI YA MIDULU
Keywords:
Simiotiki, Tamathali za semi na MsimboAbstract
Mada ya makala haya ni kuchunguza matumizi ya lugha ya tamathali za semi katika Diwani ya Midulu. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Simiotiki yenye misimo ya Kihemenitiki, Kimatukio, Kiseme, Kiishara na Kiutamaduni. Data za makala haya zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na kuchambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa kimaelezo. Matokeo ya makala haya yamebaini matumizi ya lugha za tamathali za tashibiha, sitiari, tashihisi, jazanda na lugha isiyokuwa ya tafsida.Ufundi wa kisanaa wa kutumika kwa mbinu hizi za tamathali za semi unamfanya mtafiti kuzielewa vizuri dhamira na maudhui ambayo yamefumbatwa katika mashairi ya Diwani ya Midulu.










